DEREVA KIPATO

HUU ni mkataba wa bima unaotolewa na kampuni ya bima ya Milembe Insurance (kwa ufupi kueleweka “kampuni”) baada ya mwenye bima (hususan mtu aliyesajiliwa kumiliki rasmi leseni halali & hai ya udereva wa vyombo vya moto ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kuomba, kutoa tamko na kuthibitika kulipia kiasi chote au kukubali kulipia bei kamili ya bima hii. Mwenye bima pia anaelewa kushindwa kulipia bei husika itasababisha bima kuwa batili).          

KWA SASA INASHUHUDIWA NA KUTAMBULIKA Ya kwamba vigezo na masharti pamoja na nyongeza au mabadiliko yoyote kwenye mkataba huu ndio yatakuwa muongozo rasmi ya yatakayojiri ndani ya muda halali wa bima husika ikiwemo fidia zote zilizotajwa humu. Iwapo mwenye bima ataumia jeraha la kumdhoofisha kimwili au kufariki kutokana na ajali iliyosababishwa moja kwa moja na kipekee na sababu zinazoonekana na kuthibitishwa kutokea, kampuni itamfidia mwenye bima kiasi stahiki kwa mujibu wa vikomo vya viwango vya kufidia majeraha kama ilivyoainishwa kwenye jedwali la fidia. Kwenye mkatabu huu , Ajali itaeleweka kuwa ni tukio moja ambalo husababisha jeraha la mwili ambalo halikutarajiwa na halikusudiwa na mwenye bima, hata hivyo haijumuishi tukio lolote ambalo husababisha maradhi au magonjwa.).

SEHEMU YA I - VIGEZO

SEHEMU YA I – BIMA KWA (AJILI YA) MASLAHI YA DEREVA MWENYE LESENI YA KUENDESHA CHOMBO CHA USAFIRI WA BARABARANI.  

(Mwenye bima atafidiwa na kampuni kwa kutokuwa na uwezo wa na/au kukosa fursa ya kupata kipato kwa sababu ya kuumia ulemavu wa kimwili na au kupoteza maisha uliosababishwa na

  1. yeye kuwa dereva wa chombo cha usafiri wa barabarani kilichohusika katika ajali iliyoshuhudiwa rasmi na Polisi kwa)
    1. chombo husika kugongana pamoja na/au kupinduka 
    2. kupambana na /au kuzuia wizi au uporaji wa chombo husika
    3. kuungua na moto, moto wa kulipuka utokanao na sababu tofauti na gari lenyewe, moto wa radi
  • kuwa abiria katika mojawapo ya vyombo rasmi vya usafirishaji hususan chombo cha moto cha barabarani, treni, ndege, meli ambayo imehusika katika ajali iliyoshuhudiwa rasmi.
  1. The Insured shall be entitled to compensation of maximum two (2) types of bodily injury benefits resulting from the same accident or disability period namely Medical Expenses and any of either temporary total disability, permanent disability, or death. This is subject to death happening within a year of the accident. Similarly, injury or disability becomes apparent within a year of the accident.  No further liability to compensate under this policy shall bind the Company after a claim of one of the mentioned benefits has been submitted and concluded payable.
  • Fidia ya kila wiki iliyoainishwa kwenye hati ya bima italipwa baada ya kampuni kukubali, kudhihirisha na kupata rasmi uamuzi au ushauri wa mwisho wa kimaandishi wa daktari wa hospitali kuhusu gharama na matibabu hitimisho ya upasuaji na au tiba kwa mwenye bima. Baada ya kupata ushauri au uamuzi wa kitabibu iwapo mwenye bima atakuwa amelazwa atafidiwa au atalipwa fidia ya kila wiki kwa kikomo kisichozidi jumla ya wiki 104. Ikiwa mwenye bima ni mgonjwa wa kutwa atalipwa fidia ya wiki kikomo kisichozidi jumla ya wiki 8 tangu tarehe ya kuruhusiwa rasmi kutoka hospitali.
  • Ulemavu wa kudumu na Kifo
  • Fidia itazingatia kiasi cha asilimia (%) ya jumla ya thamani ya bima kilichoainishwa kwenye mkataba au hati ya bima kwa ajili ya ulemavu wa kudumu au kifo kwa kupunguza idadi ya wiki za fidia zilizolipwa kwa ajili ya mwenye bima kuwa majeruhi). 
  • Iwapo mwenye bima amepata ulemavu wa kudumu wa kupoteza kiungo cha mwili au udhoofu wa kiungo cha mwili ambao haujainishwa katika jedwali la fidia, basi asilimia ya fidia itapimwa na kutathminiwa kulingana na uwiano na kiwango cha ulemavu utakavyodhoofisha uwezo wa mwenye bima kutekeleza majukumu ya taaluma au kazi ya yake.     
  • Ikitokea mwenye bima amepata zaidi ya aina moja wa ulemavu wa kudumu katika ajali moja, basi idadi ya asilimia elekezi ya kiwango cha fidia cha ulemavu husika katika jedwali la fidia vitajumlishwa kwa pamoja lakini wakati wowote ule jumuisho hilo halitozidi kikomo cha fidia ya 100% ya jumla ya thamani ya bima iliyotajwa kwenye hati ya bima).

Fidia Nyinginezo

  • Gharama za Matibabu Pale itakapostahili, wakati ulemavu unaendelea fidia stahiki kwa ajili gharama za matibabu italipwa hadi pale itakapofikia kikomo cha gharama ya matibabu kilichoainishwa na jedwali la fidia kwenye hati ya bima. Pia fidia hii haitoendelea au kuzidi jumla ya wiki 104 iwe kwa fidia ya matibabu pekee au ikijumuisha pamoja na fidia ya ulemavu wa kudumu, wa muda au kifo. Iwapo kampuni imejiridhisha na kukubali rasmi kuwajibika na uhalali wa jumla ya gharama za matibabu ya mwenye bima, hivyo basi kampuni itaridhia kuidhinisha kumfidia mwenye bima gharama za matibabu alizolipia iwapo mwenye bima atawasilisha stakabadhi rasmi za EFD/VFD za Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) zinahusika na matibabu hayo.  
  • Gharama za Usafiri Kufuatia ushauri na idhini rasmi ya kimaandishi wa kitabibu kutoka kwa daktari wa hospitali, na iwapo umbali kutoka kwa makazi yanayofahamika ya mwenye bima au mji anapoishi ni zaidi ya kilomita 150 kwenda hospitali nyingine, basi kampuni pale itakapobidi italipa gharama za usafiri wa 1 1(i) mwenye bima akiwa ni majeruhi wa kulazwa kutoka hospitali moja kwenda hospitali nyingine kikomo Tshs gharama ya 1,500,000/=  1(ii) mtu mmoja (1) pekee atakayetambulika rasmi kuwa ni abiria anayesafiri kwenye ndege pamoja na mwenye bima akiwa majeruhi kikomo Tshs 1,000,000/=1(iii) kupeleka mwili wa mwenye bima kuzikwa iwapo amefariki kikomo Tshs 1,000,000/=. (2) Iwapo hospitali imeidhinisha rasmi kimaandishi kumhitaji mwenye bima kurejea mara kwa mara hospitali kumtibu majeraha yake, basi kikomo cha fidia ya usafiri ni Tshs 250,000/= kama hospitali ina umbali chini ya kilomita 150 na mji anapoishi mwenye bima. Tshs 500,000/= iwapo umbali ni zaidi ya kilomita 150. Kwa ajili ya fidia yahitajika kuwasilisha stakabadhi, Ankara, tiketi rasmi za ndege; stakabadhi ya kulipa ambulance na ushahidi mwingine utakaohitajika.
  • Gharama za Malazi: Kampuni pale itakapobidi italipa gharama za malazi hadi jumla ya kikomo ya Tshs 3,000,000/= kwa mwaka mmoja wa uhai wa bima, iwapo kwa sababu ya ajali mwenye bima amekuwa majeruhi wa kulazwa kwa zaidi ya siku saba (7) mfululizo, katika hospitali iliyo na umbali wa zaidi ya kilomita 150 kutoka kwa makazi yanayofahamika ya mwenye bima au mji anapoishi. Fidia hii ni ya kulipia malazi yaliyo jirani na hospitali alikolazwa mwenye bima ili mke, watoto na/au mtu wa karibu wa mwenye bima waweze kumhudumia na kumfariji kwa urahisi.
  • Gharama za Mazishi:  Kampuni, pale inapobidi, italipa jumla ya kikomo cha Tshs 1,000,000/= kwa ajili ya gharama za mazishi ya mwenye bima ambapo sababu ya kifo ni kwa mujibu yaliyoaelezwa kwenye mkataba huu.
  • Kupoteza Leseni hai ya Udereva &/au Pasipoti hai: Iwapo imedhihirishwa ya kwamba mwenye bima hana historia ya madai ya hizi nyaraka katika miezi sita (6) ya mwanzo wa huu mkataba, kampuni itamfidia mwenye bima gharama za kulipia leseni ya udereva &/au pasipoti iliyopotea katika ajali ya chombo cha usafiri ulioshuhudiwa na wenye kumbukumbu rasmi za Polisi. Mwenye bima akiwa amelipia bima ya mwaka mmoja ataweza kudai fidia mara moja pekee kwa kipindi hicho cha uhai wa bima yake. Kampuni itafidia au kulipia gharama za kupata leseni ya udereva &/au pasipoti mpya moja kwa moja kwenye mamlaka husika ya serikali inayohusika na makusanyo ya ada za nyaraka hizo au kumlipa moja kwa moja mwenye bima
  • Muendelezo wa Leseni ya Udereva:  Mwenye bima kufidiwa rasmi gharama stahiki za muendelezo wa uhai wa leseni yake ya udereva itakayoisha karibuni, iwapo imethibitika mwenye bima hana historia ya madai katika miezi sita (6) ya mwanzo wa huu mkataba na amelipia bima ya mwaka mmoja.

SECTION II: KUTOWAJIBIKA KWA KAMPUN

Bima hii haihusiki na au haiwajibiki na kufidia ulemavu wa au kifo cha mwenye bima): -

–  (a)  unaotokana na

  • kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu
  • Mwenye bima kuwa chini ya umri mdogo rasmi wa kuendesha vyombo vya moto vya usafiri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • kushiriki katika aina yoyote ya shughuli za michezo ikijumuisha mashindano ya aina yoyote ya vyombo vya usafiri         
  • kuwa abiria kwenye & au kuendesha baiskeli       
  • kulewa pombe au madawa ya kulevya wakati wa kuendesha chombo cha moto isipokuwa matumizi ya dawa yaliyoidhinishwa na kushauriwa rasmi kutumika na daktari   
  • baada ya kumalizika kipindi cha bima ambapo mwenye bima ametimiza au kumaliza umri wa miaka 65. Hii haitohusika iwapo kuna maombi yaliyowasilishwa na mwenye bima kuendeleza mkataba wa bima hii kuthibitika kukubaliwa na kuidhinishwa rasmi kimaandishi na kampuni. 
  • (nia ya kulaghai na/au kutumia vitendo vya udanganyifu  

(b) kutokana na Matokeo ya aina yoyote ya

  • kujiua au kujaribu kujiua, kujiumiza kwa makusudi, kuumwa ugonjwa wa akili au ugonjwa wa zinaa au mengineo, kuwepo ulemavu au kasoro za kudhoofika kimwili kabla ya kuipata bima hii.
  • (a)  Uvamizi wa kivita kutoka nchi ya au za kigeni au dalili zinazofanana na mienendo ya kivita (haijalishi kuwa imetangazwa rasmi au la), vita vya wenyewe kwa wenyewe, uasi au mgawanyiko ndani ya Jeshi, maasi ya kivita, mapinduzi ya kisiasa, uchochezi wa kuasi dhidi ya Serikali tawala, uporaji wa madaraka na majeshi pamoja na au wanasiasa                              
  • Uvamizi wa kivita kutoka nchi ya au za kigeni au dalili zinazofanana na mienendo ya kivita (haijalishi kuwa imetangazwa rasmi au la), vita vya wenyewe kwa wenyewe, uasi au mgawanyiko ndani ya Jeshi, maasi ya kivita, mapinduzi ya kisiasa, uchochezi wa kuasi dhidi ya Serikali tawala, uporaji wa madaraka na majeshi pamoja na au wanasiasa.)   
  • migomo, fujo, ghasia au vurugu za kijamii)  
  • Zuio au kizuizi, unyang’anyaji, upokonyaji wa mali kwa kutumia nguvu au sheria au zoezi linalofanana na majaribio kama hayo)
  • Mafuriko, tufani, kimbunga, mlipuko wa volkeno, tetemeko la ardhi au matukio mengine yanayohusiana na uhalisia wa dhoruba kali ya hali ya hewa    
  • Madai yoyote yatakayohusishwa na mkataba huu lakini kutokana na kukosekana kwa vipengele au masharti yanayotoa mwongozo na madai ya aina hayo.)           

MASHARTI YA KUZINGATIA, KUTEKELEZWA NA KUTII NA MWENYE BIMA

  1. Tafsiri): Vigezo, masharti yaliyomo, hati ya bima pamoja na mwongozo uliopo yote yatajumuishwa kuwa ni sehemu moja ya mkataba huu wa bima. Neno au maana yoyote kwenye nyaraka hizo husika zitatafsiriwa au kueleweka kama ilivyokusudiwa
  • Mawasiliano au Taarifa Mawasiliano au taarifa yoyote itakayohusiana na mkataba huu wa bima ni lazima yawasilishwe kwenye kampuni kwa maandishi. Baruapepe na/au barua ya maandishi ndio taratibu zinazokubalika.
  • Taarifa za AjaliTaarifa kamili ya ajali ya jeraha na/au kifo lazima iwasilishwe kwa baruapepe, kimaandishi au kwa simu ndani ya masaa 48 (siku 2) baada ya tarehe ya tukio hilo. Ucheleweshaji usio wa lazima wa mwenye bima au mwakilishi wake wa kutoa taarifa uliozidi mwezi mmoja (1) kuanzia tarehe ya kuumia kimwili/kupata jeraha & au kifo unaweza kulazimisha kampuni kufuta madai hayo. Ili kuweza kushughulikia madai ndani ya muda muafaka ni muhimu mwenye bima na/au mwakilishi wake rasmi kutoa ushirikiano mzuri kwa kampuni ya bima pale atakavyotegemewa au kuombwa kufanya hivyo.
  • Ushahidi Taarifa na Ushahidi wote unaohitajika na kampuni utawasilishwa na mwenye bima au mwakilishi wake rasmi kwa gharama zake binafsi kwa mujibu wa jinsi kampuni itakavyozihitaji na kupendekeza. Ripoti ya maendeleo ya kitabibu kuhusiana na jeraha na/ au ulemavu husika ni lazima itawasilishwa kwenye kampuni na mwenye bima kadiri itakavyohitajika.
  • Usiri/Taarifa binafsi Pale inapohitajika kampuni yaweza kuhitaji kukusanya au kutumia taarifa binafsi za mwenye bima kwa lengo kuu la kuboresha ubora wa huduma za bima, usimamizi na utekelezaji wa taratibu za bima, kushughulikia na kutathmini madai, kufanya utafiti yakinifu na kubuni huduma mpya za bima. Kampuni yaweza kushindwa kutoa huduma ya bima au kushughulikia madai iwapo mwenye bima hatowasilisha taarifa zinazostahili na zilizo sahihi kwa kampuni. Kwa kuwasilisha taarifa itatambulika mwenye bima ameridhia kwa kampuni pale inapobidi kutoa taarifa hizo kwa kampuni zingine za bima, madalali au mawakala wa bima, kampuni za bima mtawanyo, mfumo wa ushirikishwaji wa taarifa za mikopo na za bima, washauri wa kampuni, wachunguzi na watathmini wa madai ya bima, benki, serikali, vyombo vya dola, usuluhishi, taasisi za serikali za uratibu na usimamizi au pale inapohitajika kisheria)
  • Uchunguzi Iwapo mwenye bima amefariki kampuni kwa gharama zake yenyewe ina haki ya kufanya upasuaji wa mwili kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo 
  • Muendelezo wa Bima:  Pale inapotokea mwenye bima anahitaji kulipia bima hii kwa ajili ya muendelezo wake, basi mwenye bima anapaswa kuthibitisha na kuwasilisha kimaandishi kwenye kampuni iwapo tangu tarehe ya mwisho alipie bima hii na/au tarehe ya bima ya awali ilipoisha kama ameshapata jeraha la kumdhoofisha kiungo cha mwili, ulemavu au ugonjwa wa aina yoyote.
  • Kusitisha Bima): Kampuni inaweza kusitisha mkataba wa bima kwa kutoa taarifa rasmi kwa mwenye bima kwa kutumia baruapepe, SMS, whatsapp na au barua ya maandishi ya kumfahamisha mwenye bima au kuhusu nia hiyo. Taarifa au notisi ya siku ya kusitisha bima huwa inakuwa ni siku saba (7) tangu tarehe ya kuandika taarifa au notisi hiyo. Kutokana na kusitishwa kwa mkataba wa bima au bima yenyewe, kampuni italazimika kumrejeshea mwenye bima pesa stahiki anazopaswa kurudishiwa mwenye bima kulingana na muda ambao bima hiyo haijatumika tangu tarehe ya kusitisha bima hiyo hadi tarehe ya kuisha bima hiyo. Marejesho ya pesa hizo kwa mwenye bima yatawezekana, iwapo itathibitika ya kwamba kabla ya tarehe ya kusitisha bima hiyo mwenye bima hakuwahi kudai fidia tangu tarehe ya kuanza na hadi ya kusitisha bima husika. Ili mwenye bima arejeshewe pesa stahiki ni lazima kwanza arudishe hati, mkataba, na stakabadhi ya malipo ya bima.
  • Majukumu ya mwenye bima Muda wote inatarajiwa mwenye bima kutii na kutekeleza vigezo na masharti yaliyomo kwenye bima au mkataba huu. Pia ni jukumu la mwenye bima muda wote kuijuza na kupaswa kujibu, kuwasilisha kwenye kampuni taarifa zilizokamilika, sahihi, na za ukweli kuhusiana na hali yake kabla ya kupata bima na wakati wa uhai wa bima husika. Ukweli, usahihi wa taarifa hizo pamoja na uwajibikaji wa utekelezaji wa vigezo na masharti husika wa mkataba huu ni moja ya sababu kubwa zinazothaminiwa na kuchunguzwa na kampuni ya bima kabla ya kufanya maamuzi ya kulipia fidia ya aina yoyote ile.
  1. Uwakilishi na Utetezi Kampuni kwa hiari yake  
    1. itaandaa au kuteua mwakilishi kwa ajili ya uchunguzi wa kina wa madai ya fidia ya ulemavu na au kifo cha mwenye bima yatakayohusiana na bima hii.)
    1. itaamua kujitetea kwenye mahakama yoyote dhidi madai ya fidia yanayoshukiwa kusababisha au kuhusiana na tukio lolote linalodhaniwa kutakiwa kufidiwa na bima hii.)
  1. Mahakama) Bima hii itaongozwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni mahakama pekee za Tanzania zitakuwa na mamlaka juu ya kesi yoyote itakayohusiana na bima hii).

Loss of or Permanent Disablement                                % of Maximum Benefit Payable 

M/mikono au Ki/Viganja…………..……………………………………………………………..………………………………………………………100%  

Miguu au Nyayo)...............……………………………………………………100%  

Kutokuona macho yote) ........………………………………………………..100%  

Kutosikia masikio yote)...…………............................................100%  

mkono/kiganja au mguu/unyayo & kuwa kipofu)..100%

(mkono/kiganja au mguu/unyayo & kuwa bubu) 100%

Ukichaa usiotibika).............................................100%

Kupooza milele kwa mguu na/au mkono)...…………100%  

Kifo)............................................................………………………………………………..100%

Jicho moja kutokuona milele).........................50%

Sikio moja kutosikia milele)……….……………...10%    

Kidole au Vidole Gumba) ....................……………..………………………..20%

(Kidole kidogo au Vidole vidogo zaidi)………………..……………….15%

Kidole chochote kasoro gumba na kidogo)……………………...6%   

Kidole kikubwa cha Mguu)..…………………………………………………………..5%

Kidole kidogo cha Mguu)...…………………………………………………………3%